MOI yaendesha mafunzo ya tisa ya matibabu ya mifupa na majeruhi wa ajali kwa wataalam kutoka Afrika mashariki, kati, kusini na magharibi MOI


Na Abdallah Nassoro-MOI
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inaendesha mafunzo ya Tisa ya siku nne ya matibabu ya kibingwa na kibobezi ya majeruhi wa ajali kwa madaktari bingwa wa mifupa kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, Kati Kusini na Magharibi.
Mafunzo hayo maefunguliwa leo Juni, 04, 2024 na Mkurugenzi matibabu ya mifupa na ajali wa MOI Dkt. Antony Assey ambaye amesema mafunzo hayo yamelenga kubadilishana uzoefu juu ya njia mpya na bora za kutibu majeruhi wa mifupa na ajali.
“Wote tunafahamu kuwa MOI ni kituo cha umahiri cha matibabu ya mifupa na majeruhi wa ajali na kwamba mafunzo haya yataboresha matibabu ya mivunjiko ya mifupa na magonjwa yatokanayo na ajali kwa nchi za kusini mwa jangwa na Sahara kwa kubadilisha mbinu bora na mpya za matibabu zinazotawala duniani kwa sasa” amesema Dkt. Assey na kuongeza kuwa
“MOI inatoa shukrani za dhati kwa taasisi ya SIGN fracture Care International kwa ushirikiano wao katika kuijengea uwezo wa matibabu ya mifupa mirefu…ushirikiano wao umewezesha MOI kuwa kituo cha umahiri kwa matibabu Afrika Mashariki na kati, pia niwashukuru washirika wa mafunzo haya taasisi ya kimataifa ya mifupa na ajali (Institute of Global Orthopaedics and Traumatology- IGOT), AO Alliance na chuo kikuu cha California San Francisco (UCSF)
MOI imekuwa ikipokea wagonjwa wengi kutokana na ongezeko la ajali katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kunakosababishwa na ongezeko la vyombo vya moto na uwingi wa watu, hii imechangia MOI kuwa miongoni mwa taasisi za kwanza duniani kupokea idadi kubwa ya majeruhi wa ajali”
Kwa upande Mratibu wa Mafunzo hayo daktari bingwa wa mifupa kutoka MOI Dkt. Joseph Mwanga amesema mafunzo hayo yaliyoshirikisha zaidi ya wataalam 100 yamejikitaka kinadharia na vitendo ambapo kada zote za udaktari kuanzia wa ngazi ya chini hadi juu watanufaika.
“Kuna madaktari bingwa wa mifupa kutoka nchi za Afrika Mashariki, Kati, Kusini na Magharibi…katika mafunzo yetu haya ya Tisa watalaam watabadilishana uzoefu katika njia bora na za kisasa za tiba ya mifupa na majeruhi wa ajali, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora” amesema Dkt. Mwanga na kuongeza kuwa.
“Wawezeshaji wametoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani, Gambia, Nigeria na Kenya huku wakishirikiana na wabobezi wazawa wa Tanzania kutoka taasisi ya MOI”.

About the Author

You may also like these