Mbagala Epiphan hospital

MOI yasogeza huduma za kibingwa kwa wakazi wa Mbagala

Na Mwandishi wetu MOI,

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI inaendelea kutekeleza agizo la serikali ya awamu ya sita la kusogeza huduma zake za kibingwa kwa wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo leo zaidi ya wagonjwa 150 wamehudumiwa katika Hospitali ya Epiphany Mbagala.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Anthony Assey amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea kuipa kipaumbele Sekta ya Afya hivyo ni muhimu kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi.

“Leo tuko hapa Mbagala katika hospitali ya Epiphany ambapo tunashirikiana na wenzetu wa hospitali hii kusogeza huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kwa wananchi ili kuwaondolea usumbufu wa kufuata huduma MOI kupitia kwenye huduma yetu ya kliniki jongefu (MOI Mobile Clinic). Alisema Dkt. Assey.

Kwaupande wake Mkurugenzi mtendaji wa Epiphany Bw.Pharles Yikobela ameishukuru na kuipongeza taasisi ya MOI kwa kuanzisha huduma ya kliniki jongefu (MOI Mobile Clinic) ili kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi

“Niwaombe MOI wasiishie tu hapa, waendelee kuja tena na tena kwenye Hospitali yetu ya Epiphany ili wananchi waendelee kunufaika na programu hii ya Kliniki jongefu” Alisema Yikobela.

Naye Daktari Bingwa wa Mifupa Dkt. Bryson amewaasa wananchi kuendelea kuchangamkia fursa ya huduma za kliniki jongefu ya MOI kwani ni fursa ya kipekee kwa wananchi kupata huduma za kibingwa za MOI bila kulazimika kufika MOI.

Mkazi wa Mbagala Bi. Husna Ramadhani ameushukuru uongozi wa MOI pamoja na Epiphany kwa kutusogezea huduma za kibingwa katika eneo la Mbagala kwani imesaidia kuwapunguzia gharama na usumbufu kwa wananchi kufuata huduma MOI.

About the Author

You may also like these