MOI yasogeza huduma za kibingwa kwa wakazi wa Mbagala

Wafanyakazi 500 wameshiriki mkutano wa mwaka wa watumishi wa MOI

Mwandishi wetu MOI,

Mkutano mkuu wa mwaka kati ya uongozi na watumishi wote wa MOI umefanyika leo katika ukumbi wa L5 katika chuo kikuu MUHAS ambapo zaidi ya watumishi 500 wamehudhuria.

Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema mkutano huu umefanyika kwa lengo la kujenga uelewa na pamoja kati ya Watumishi na menejimenti ili kuendelea kuboresha hali ya utoaji huduma za kibingwa kwa mgonjwa.

“Leo ni siku pekee katika Taasisi yetu ya MOI ambapo tumefanya kikao muhimu na kizuri kati yetu sisi viongozi na Watumishi wenzetu tumejadiliana kwa kina na naamini mawazo yaliyotolewa ni ya kujenga na kitaleta mageuzi chanya “ Alisema Dkt Boniface

Dkt Boniface amesema menejimenti ya MOI imejikita katika maamuzi shirikishi na yeye uwazi ili kila mtumishi wa MOI awe na mchango katika mafanikio ya Taasisi ya MOI.

Kwa upande wake,mwenyekiti wa TUGHE MOI Bw. Privatus Masula ameushukuru uongozi na MOI kwa kuendelea kuiitisha mikutano na wafanyakazi kwa lengo la kufanya maamuzi pamoja.

Naye Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu MOI Bw. Orest Mushi amesema mikutano kati ya menejimenti na watumishi wote ipo kisheria na inafanyika ili kujenga uelewa wa pamoja kati ya menejimenti na watumishi wote.

Watumishi wa MOI wamepongeza uwepo wa mkutano huu ambapo wametoa maoni, madukuduku na ushauri kwa lengo la kuendelea kuboresha mazingira ya kazi na huduma kwa wagonjwa.

About the Author

You may also like these