MKUU WA MKOA WA TABORA

Mkuu wa mkoa wa Tabora aipongeza MOI kwa kusogeza huduma za kibingwa kanda ya Magharibi

Na Mwandishi wetu- Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Balozi, Dkt. Batilda Salha Burian amefanya ziara ya kikazi katika kambi maalum ya matibabu ya kibingwa na bobezi ya Mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu inayoendesha na Madaktari bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) wakishirikiana na Madaktari bingwa wa hospitali ya Rufaa Nkinga, Tabora.

Akizungumza katika ziara hiyo Dkt. Batilda amewapongeza Madaktari bingwa bobezi wa MOI kwa kusogeza huduma za kibingwa kwa wakazi wa magharibi.

“Nimefurahi kuwaona Madaktari bingwa wa MOI katika hospitali hii ya rufaa Nkinga wakitoa huduma kwa wagonjwa wenye magonjwa ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu wakishirikiana na wenyeji wao, hongereni kwa kusogeza huduma zenu kwani mmewapunguzia mzigo wa gharama za kufuata huduma hizo Dar es Salaam”. Aisema Dkt. Burian

Kwa upande wake Daktari bingwa wa Ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kutoka MOI Dkt. Alpha King’omela amesema kambi hii ya matibubu ni matokeo ya mahusiano mazuri baina ya Taasisi ya MOI na hospitali ya Rufaa ya Nkinga ambapo lengo ni kuhakikisha wakazi wa magharibi wanapata huduma hizo za kibingwa na kibobezu kwa gharama nafuu.

Naye, Mkazi wa Shinyanga Bi. Rebeca Charles ameshukuru Serikali kwa huduma bora zinazotolewa katika kambi hiyo na kuwataka Watanzania waendeee kujitokeza kwa wingi katika kambi hiyo.

Hii ni sehemu ya mkakati wa Taasisi ya MOI wa kutekeleza agizo la Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha huduma za kibingwa za mofupa, ubongo , mgongo na mishipa ya fahamu zinasogezwa karibu na wananchi.

About the Author

You may also like these