MOI yafanya upasuaji wa kurekebisha kibiongo kwa watoto.

Na Mwandishi wetu- MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imewafanyia upasuaji wa kurekebisha kibiongo watoto 10 kwa mafanikio makubwa katika kambi maalum iliyoendeshwa na madaktari bingwa wa MOI kwa kushirikiana na Madaktari bingwa kutoka Marekani , Italia, Palestina na  Umoja wa Falme za Kiarabu.

Kambi hii ilianza Februari 5 hadi 9, 2024 ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mpango mkakati wa MOI wa kuwajengea uwezo wataalam wa ndani ili wawe mahiri katika kurebisha migongo iliyopinda (Scolliosis) iliyoanza mwaka 2017.

Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo katika vyumba vya upasuaji MOI ,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Lemeri Mchome amesema kuanza kwa huduma hii hapa nchini kumesaidia Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingetumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi.

“Gharama za upasuaji wa kunyoosha mgongo uliopinda (Kibiongo) kwa mtoto mmoja ni katika ya milioni 15 hadi 17 lakini nje ya nchi gharama zinafika hadi Tsh milioni 60” amesema Dkt. Mchome

Kwaupande wake mkufunzi kutoka nchini Palestina Prof. Alaa Ahmad amesema mafunzo hayo yamelenga kuiwezesha MOI kuwa kituo cha umahiri katika matibabu ya kurekebisha mgongo Afrika Mashariki, kati na kusini.

“Mafunzo haya ya umahiri katika kufanya upasuaji wa kurekebisha kibiongo yataiwezesha MOI kuwa kituo cha umahiri cha kutibu na mafunzo Afrika Mashari na Kati na kusini ambapo wataalam wao hujifunzia hapa MOI” amesema Prof. Alaa.

Taasisi ya MOI ni kituo cha umahiri cha Chuo cha Madaktari bingwa wa upasiaji cha Afrika Mashariki , kati na Kusini (COSECSA)cha kufundishia madaktari bingwa wa Mifupa , Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu.

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these