MOI wamlilia Prof. Philemoni Sarungi, mmoja wa waanzilishi wa taasisi hiyo

Na Mwandishi wetu- Dar es Salaam

Viongozi na watumishi kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wameungana na mamia ya waombelezaji wengine kumlilia na kumuombea aliyekuwa mmoja wa waanzilishi wa Taasisi hiyo Prof. Philemoni Mikol Sarungi katika tukio la kuaga mwili wake liliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo limefanyika leo Siku ya jumatatu tarehe 10 Machi, 2025 katika viwanja vya Karimjee ambapo watumishi wa MOI pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali walifika kuaga mwili wa Prof Sarungi ambaye alifariki Siku ya tarehe 05 Machi, 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amemshukuru Prof Philemon Sarungi kwa kutengeneza njia ya ubobezi katika upasuaji wa Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Ufahamu kwa madaktari hapa Tanzania.

“Leo tuna wataalam waliojitika katika mfumo mzima wa fahamu kuanzia kwenye Ubongo, Uti wa mgongo, Mishipa ya fahamu na kwa aina zote za magonjwa hayo kwa sababu ya Prof. Philemon Sarungi kwani ni yeye ambaye alitengeneza njia na kutuheshimisha mpaka siku ya leo MOI imeweza kusimama na itaendelea kusimama katika kutoa Huduma za kibingwa na kibobezi wa Upasuaji wa Mifupa kwa Wananchi” alisema Dkt. Mpoki na kuongezea

“Sisi kama taasisi tutaendelea kuenzi maono yake na uthubutu wake na hakuna siku ambayo itapita hatutokumbuka kwamba alikuwepo shujaa aliyeanzisha fani hii hapa nchini….Taasisi ya MOI inashukuru kwa yale yote ambaye Prof. Philemon Sarungi aliyofanya katika taasisi yetu na nchi nzima kwa ujumla, tutaendelea kuenzi uhodari wake na uthubutu wake”.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe Amen.

About the Author

You may also like these