MOI kufanya upasuaji wa kurekebisha kibiongo watoto 20

Na Abdallah Nassoro-MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inatarajia kuwafanyia upasuaji wa kurekebisha kibiongo watoto 20, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa ndani chini ya usimamizi wa watalam kutoka Palestina, Italia na India.

Upasuaji huo utakaofanyika katika mfululizo wa kupeana ujuzi katika nyanja hii ya mgongo. Vibiongo ni muendelezo wa programu ya mafunzo iliyoanza mwaka 2017 yenye lengo la kuwajengea uwezo madaktari wazawa kuwa mahiri katika kurebisha tatizo hilo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mkurugenzi wa huduma za Upasuaji wa Ubongo Dkt. Lemeri Mchome amesema leo Februari 5, 2024 kuwa mafunzo hayo yalianza kwa njia ya mtandao mwaka 2017 na 2019 kambi ya kwanza ya upasuaji ilifanyika ambapo wagonjwa 5 walifanyiwa upasuaji kwa mafanikio makubwa. Kambi ya pili ilifanyika mwaka 2022 ambapo pia wagonjwa 8 walifanyiwa upasuaji na watoto zaidi ya 20 kufungwa POP maalum la kuzuia kibiongo kisiendelee. Mwaka 2023 matibabu mapya ya hatua ya kwanza kwa vibiongo vilivyojikunja sana yalianzishwa hapa kwenye Taasisi ikiwa ni tiba ya kwanza inayotolewa Afrika mashariki, kati na kusini. Kwa kambi hii ya sasa tunaenda katika hatua ya pili ya matibabu ambayo ni upasuaji.

“Baada ya mafunzo haya wataalamu wetu wataendelea na kutoa huduma hizi kwa kiwango cha kimataifa.
Hivyo nitoe wito kwa watanzania wenzangu kuwaleta wagonjwa mapema ili wafanyiwe uchunguzi mapema na kuanzishiwa matibabu.

Kwa upande wake Prof. Alaa Ahmad kutoka Palestina mafunzo hayo yatawawezesha kuwa wabobezi na kutoa mafunzo kwa madaktari wengine wa hospitali za rufaa na kuwa kituo cha umahiri wa matibabu ya kurekebisha kibiongo Afrika Mashariki.

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these