Na Amani Nsello-MOI.
Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) leo Agosti 27, 2024 wamepewa mafunzo ya kuchukua taadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa MPOX ambao umesambaa katika baadhi ya nchi jirani.
Mkuu wa kitengo cha dharura cha MOI Dkt. Edson Francis amesema licha ya kuwa ugonjwa huo haujaingia nchini, ni muhimu kwa watumishi wa MOI kuanza kuchungua taadhari kutoka na kuwa katika mjumuiko wa watu wengi.
“Hapa hospitalini kwetu kuna muingiliano mkubwa wa watu mbalimbali, hivyo sisi kama watumishi tunapaswa kuchukua tahadhari na kujikinga na ugonjwa MPox ingawa hapa kwetu (nchini) haujaingia, ugonjwa umeripotiwa nchi jirani za Kongo na Burundi,”. Amesema Dkt. Edson
“Epukeni kushikana mikono, lakini pia kumbukeni kunawa mikono kila mara kwa maji safi na kitakasa mikono (Sanitizer), sisi ni taasisi ya afya hivyo ni muhimu kwetu kuhakikisha watumishi wote wanapewa elimu hii muhimu kwa ajili ya kujikinga na virusi hivyo” amefafanua
Dkt Edson amesema MPOX ni ugonjwa wa virusi unaopatikana kwa wanyama wakiwemo nyani, kutokana na mwingiliano wa shughuli za kibinadamu ambapo virusi vya ugonjwa huo vinaweza kuhamia kwa binadamu kutoka kwa wanyama hao.
Awali Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Fidelis Minja amesema ni muhimu kwa watumishi wa MOI kuchukua taadhari mapema kutokana na kuripotiwa kusababisha vifo katika nchi ambazo ugonjwa huo umeripotiwa.