Menejimenti ya MOI yakagua maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za ndani na kuanza kutatua changamoto zilizopo.

Na Mwandishi wetu- MOI

Menejimenti ya Taasisi ya tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) leo imepita na kukagua maeneo mbalimbali ya kutolea huduma pamoja , hasa wodini kwa Wagonjwa na ndugu na miradi ya maendeleo ndani ya Taasisi kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali na kuzitatua hapo hapo.

Menejimenti hiyo imefanya zoezi hilo leo mchana hadi jioni tarehe Februari 11, 2024 ambapo imetembelea kitengo cha dharura, kitengo cha wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (HDU), wodi za wagonjwa wa kawaida na za kulipia.

Timu ya Menejimenti ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi , Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Madaktari na Wauguzi wafawidhi imetoa msisitizo mkubwa katika ubora wa huduma kwa wananchi pamoja na mawasiliano bora kati ya wateja na watoa huduma.

Menejimenti imeelekeza Watalamu Mabingwa na Wasaidizi wao kutenga muda wa kuwasiliana na kutoa mrejesho wa matibabu kwa wagonjwa na ndugu wawili walioridhiwa na mgonjwa.

Aidha , menejimenti imeagiza kuondoa kero za wagonjwa kuchelewa kufanyiwa upasuaji au kuahirishwa bila sababu za msingi. Maelekezo yametolewa kwa wakuu wa Idara kuhakikisha wagonjwa walioahirishwa operation na waliokaa muda mrefu wafanyiwe kuanzia wiki ijayo kama wameshakuwa tayari kufanyiwa upasuaji baada ya kukamilisha taratibu zote .

Ikiwa katika mradi wa maboresho ya vyumba viwili vya upasuaji vya kitengo cha dharura menejimenti ya MOI imemuagiza Mkandarasi huyo kukamilisha mradi huo kabla ya tarehe 28/ 02/ 2024 kwa sababu upungufu wa vyumba vya upaauajo kwa sasa ni tatizo linalochangia baadhi ya operation kuahirishwa.

“Nawakumbusha viongozi wenzangu tufungamane wote katika mstari mmoja wa kuwahudumia wananachi pamoja na kiongozi akitoa maagizo unapaswa kuyapokea, unampa muda wa kuyatekeleza na kutoa mrejesho ukipewa maagizo usikae kimya” amesema Prof. Makubi

Aidha, Prof. Makubi amewapongeza wajumbe wa Menejimenti kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha wanaendelea kuboresha huduma za kibingwa na kibozi za MOI ijapokuwa bado kuna changamoto za kuzifanyia kazi lakini anathamini jitihada zao wanazozifanya katika Taasisi hiyo. Menejimenti pia imepokea changamoto za miundombinu katika baadhi ya wodi , vitanda na kuahidi kuendelea kuziboresha.

kwa upande wao wateja waliohojiwa na wajumbe wa menejimenti katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma wamekiri kuridhishwa na huduma wanazozipata MOI na kuwashukuru watoa huduma wa MOI kwa huduma nzuri wanazotoa.

About the Author

You may also like these