MENEJIMENTI MOI YAHIMIZWA KUDUMISHA USHIRIKIANO KATIKA UTOAJI WA HUDUMA


Abdulaziz Seif -MOI

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Dkt Lemeri Mchome ameihimiza menejimenti kutekeleza majukumu yao kwa kushirikiana ili kuhakikisha taasisi inaendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi.

Dkt. Lemeri ametoa rai hiyo leo Julai 30,2024 wakati wa majumuisho ya ukaguzi wa hali utoaji huduma na miundombinu (Grand round) ili kutathimini hali ya utoaji huduma kwa wananchi.

Amesema kuwa kama viongozi wakishirikiana kwa pamoja na kuwa naa malengo yanayofanana basi ni rahisi kwa Taasisi kufikia malengo yake hususani kutoa huduma bora za kibingwa na kibobezi.

“Ni wajibu wetu kushirikiana katika majukumu yetu ya kila siku, kwa kila utaratibu tutakaouweka sisi kama viongozi tuwe wakwanza kuhakikisha utaratibu huo unatekelezwa kwa mfano malengo yetu ni kufanya upasuaji watu 40 kwa siku hii itawezekana kama kila kiongozi atawajibika kwa nafasi yake”

Pia Dkt Lemeri Mchome ameipongeza menejimenti kwa kusimamia viziri utoaji wa huduma kwa wagonjwa haswa waliolazwa wodini.

“Kuhusu utoaji wa huduma nawapa pongezi sana, sisi wote tumekuwa mashahidi tulipopita wodini kila mgonjwa tuliemuuliza kuhusu ubora wa huduma ametoa pongezi kwa madaktari pamoja na manesi, hakuna alielalamika kuwa amecheleweshwa kufanyiwa upasuaji, mazoezi tiba, kupewa dawa au matibabu mengine”

Pia alizungumzia changamoto zilizopo za miundombinu na msongamano wa wagonjwa katika eneo la wagonjwa wa nje kwa kuelezea jitihada za wizara ya Afya katika kutekeleza Mradi wa ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje unaotarajiwa kuanza siku za usoni kama suluhisho la kudumu.

Aidha miundombinu chakavu itarekebishwa kwa awamu ili kuhakikisha mazingira ya kuvutia kwa wafanyakazi na wagonjwa.
Baadhi ya maeneo ambayo timu ya Menejimenti imetembelea ni Wodini, Kitengo cha dharura, chumba cha upasuaji (Theatre), ICU pamoja na HDU.

About the Author

You may also like these