Madaktari bingwa wazawa watakiwa kuwajengea uwezo wenzao

Na Amani Nsello- MOI

Madaktari Bingwa na Wabobezi wazawa wamehimizwa kuwajengea uwezo wa kutoa huduma za upasuaji wa kuongeza urefu wa mifupa na kurekebisha ulemavu madaktari wengine katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza ufanisi wa tiba za kibobezi.

Wito huo umetolewa leo Alhamis Novemba 28, 2024 na Daktari Bingwa Mbobezi wa upasuaji wa mifupa kutoka Chuo Kikuu cha Manchester cha nchini Uingereza, Dkt. Amer Shoaib wakati wa kufunga kambi ya mafunzo katika Taasisi ya MOI.

Dkt. Shoaib amewataka Madaktari hao bingwa na wabobezi wazawa waliohudhuria kambi hiyo ya mafunzo kutumia elimu hiyo waliyoipata kuwafundisha madktari wenzao wazawa ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

“Inatakiwa mtumie elimu hii mliyoipata hapa kuwafundisha wenzenu ambao hawakuhudhuria mafunzo haya, itawasaidia na wao kuweza kuongeza ujuzi na mbinu za kufanya upasuaji wa kuongeza urefu wa mifupa na kurekebisha ulemavu… Kwa kufanya hivyo itawasaidia kutoa huduma bora ya matibabu kwa wagonjwa “- amesema Dkt. Shoaib

Kwa upande wake, Meneja wa Idara ya Upasuaji na Maungio wa MOI, Dkt. Violet Lupondo, ameishukuru Menejimenti ya Taasisi ya MOI kwa kuwapa ukumbi kwa ajili ya kuendesha kambi hiyo ya mafunzo pamoja Madaktari Bingwa kutoka nchini Uingereza kwa kuwezesha mafunzo hayo

About the Author

You may also like these