Madaktari bingwa na wabobezi kutoka uingereza wapiga kambi MOI kuwanoa madkatari wazawa

Na Amani Nsello- MOI

Madaktari Bingwa na Wabobezi kutoka nchini Uingereza wamepiga kambi ya mafunzo katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kuwanoa Madaktari wazawa juu ya upasuaji wa kuongeza urefu wa mifupa na kurekebisha ulemavu.

Kambi hiyo imefunguliwa leo Jumatatu Novemba 25, 2024 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Lemeri Mchome huku yakihudhuriwa na madaktari wa mifupa kutoka hospitali ya rufaa za kanda nchini.

Kambi hiyo yenye malengo ya kuboresha mbinu za upasuaji wa kurefusha miguu na mikono na kurekebisha ulemavu unaotokana na sababu mbalimbali zikiwemo ajali za barabarani  na kusababisha mguu au mkono kuwa mfupi.

Akifungua kambi hiyo ya mafunzo, Dkt. Lemeri amesema kuwa MOI wamekuwa wakitoa huduma za upasauji wa mifupa kwa zaidi ya miaka 20, lakini kupitia kambi hiyo, mafunzo hayo yatawaongezea ujuzi na mbinu za upasuaji wa kurefusha miguu na mikono.

“MOI tumekuwa tukitoa huduma za upasuaji wa mifupa kwa zaidi ya miaka 20 sasa, lakini naelewa kambi hii ya mafunzo inajumuisha madaktari Bingwa na Wabobezi kutoka Hospitali za kanda na zile za Mikoa za Rufaa…. Kupitia kambi hii mtapata ujuzi na mbinu ambao zitawasaidia kufanya upasuaji wa mifupa wa kibobezi zaidi”-amesema Dkt. Lemeri

Kambi hiyo ya mafunzo ya siku 3 imeanza leo Novemba 25, 2024 na itafikia tamati Novemba 28, 2024 na Wakufunzi wa mafunzo hayo ni Madaktari Bingwa na Wabobezi kutoka Chuo Kikuu cha Uingereza wakiambatana na Madaktari Bingwa wazawa wanaoongozwa na Meneja wa Idara ya Upasuaji wa Mifupa na Maungio, Dkt. Violet Lupondo ambaye amebainisha kuwa upasuaji huo unatumia mbinu ya vyuma vinavyoonekana kwa nje vyenye umbo la duara (Ilizarov Rings).

About the Author

You may also like these