Na Radhia Balozi, MOI
Watumishi 50 wa Taasisi ya tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wanapewa mafunzo ya kuongeza uelewa wa kukinga na kudhibiti maambukizi ili wawe salama katika maeneo ya kutolea huduma za afya.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika MOI na yalifunguliwa na mwakilishi wa MOI Dkt. Asha Abdullah ambaye aliwaasa washirki kuzingatia kutokana maambukizi kuwa ni moja ya vyanzo vinavyoongoza katika kusababisha maradhi ya vifo nchini Tanzania.
“Mafunzo haya ni ya siku tatu yanalenga kukinga watoa huduma za afya dhidi ya maambukizo katika maeneo ya kutolea huduma za afya (Health Care Associated Infection), kuwapa watoa huduma za afya marejeo ya haraka ya mambo ya msingi kuhusu mienendo inayofaa kukinga na kudhibiti maambukizi kwa njia iliyorahisi na inayooleweka” amesema Dkt. Asha
Pia, Dkt. Asha amesema wanatarajia baada ya mafunzo haya watoa huduma wa MOI watafuatilia jinsi ya kujikinga na kuwakinga wagonjwa dhidi ya maambukizi katika maeneo ya kutolea huduma za afya.
“Mafanikio yetu katika kuijenga MOI mpya, yanategemea namna tutakavyoimarisha ushirikiano wetu katika utekelezaji wa dhana hii ya kukinga na kudhibiti maambukizi” amesema Dkt. Asha
Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo haya Bi.Zaituni Bembe amewahimiza watumishi wa MOI kuendelea kuchukua tahadhari ili wafanyakazi na wagonjwa kuendelea kuwa salama.