Wauguzi MOI wapewa mafunzo ya malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto

Na Amani Nsello-MOI.

Wauguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wamepewa mafunzo ya malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto ili kutoa uelewa wa pamoja namna bora ya kulea na kutoa uangalizi wa watoto.

Mafunzo hayo yametolewa leo Jumatano Agosti 14, 2024 na Afisa Ustawi wa Jamii wa MOI, Stella Kihombo ambaye amesema umuhimu wa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa malezi bora kwa watoto  kwa kuwa muda mwingi wanautumia kazini hivyo hukosa muda wa kukaa na kuwalea watoto nyumbani.

“Asubuhi unaamka unawaza foleni barabarani, mtoto umemuacha nyumbani kazini hujasaini kwenye Biometric, Jumatatu upo kazini unaunganisha hadi Alhamisi asubuhi ndiyo unarudi nyumbani”. Alisema Stella Afisa Ustawi wa Jamii.

Aidha, Stella ametolea ufafanuzi wa nyanja za malezi ambazo ni Kiroho, Kijamii, Kimwili, Kiakili na Kisaikolojia. Pia aliwaeleza Wauguzi aina mbalimbali za malezi kama vile; Malezi ya kutumia mamlaka (Dictatorship), Malezi ya kuongoza (Democracy), Malezi ya kuruhusu (Laizess Faire) na Malezi ya kutojihusisha (Non Involvement).

Amewaasa watumishi hao kuwa haijalishi majukumu mengi ya kazi waliyonayo ya Kutumikia Umma, wanapaswa kutenga muda wa kukaa na watoto wao kwa kuwaelekeza, kuwakanya na  kuwaonya masuala mbalimbali ya Kijamii.

About the Author

You may also like these