Watumishi wa MOI wajipanga kuwa kinara utoaji huduma bora za mifupa na ubongo barani Afrika

Na Mwandishi Wetu-MOI 12, Agosti 2023

Watumishi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wamejipanga kutoa huduma bora kwa wagonjwa ili kufikia adhma yake ya kuwa kinara wa tiba za kibingwa na kibobezi za Mifupa, Ubongo, mishipa ya fahamu na mafunzo barani Afrika.

Hayo yamebainishwa katika Mkutano mkuu wa Menejimenti na watumishi wote MOI katika ukumbi wa CPL Muhimbili kwa lengo la kuboresha huduma.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI ,Prof. Makubi amesema ili kuindoa MOI kutoka kutoa huduma bora hadi bora zaidi za kimataifa ni wajibu wa kila mfanyakazi kutimiza wajibu wake kwa kuzingatia kwa kuzingatia maadili na weledi wa Hali ya juu.

“Lengo letu ni kutoa huduma bora za tiba ya mifupa, Ubongo, mishipa ya fahamu na mafunzo katika bara Afrika” na kuifanya Taasisi ipunguze utegemezi wa kifedha toka serikali kuu ;alisema Prof. Makubi

Naye Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala MOI Bw.Orest Mushi amesema maboresho hayo yatagusa maslahi ya watumishi hivyo ni wajibu wa kila mmoja kutimiza wajibu wake, kufikia malengo ya kutoa huduma kila kitengo na kuondoa kero kwa Wagonjwa

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyazi wa Afya Serikali (TUGHE) tawi la MOI, Privatus Masula amewataka wafanyakazi hao kujituma kuongeza kila huduma, kasi ya utendaji na pia mapato ya taasisi ili wapate maslahi mazuri zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa fedha Bi.Veronica Nyahede amesema ili kuyafikia malengo hayo MOI imepanga kuhakikisha tunafikia malengo ya kupata fedha gharama za huduma zote , uendeshaji na motisha Kwa Watumishi.

Baadh ya watumishi walishauri menejimenti kuwekeza kwenye utaalam na vifaa tiba , dawa, vifaa vya upasuaji ili wagonjwa wengi wapate huduma bora na kwa haraka na waliahidi kutoa ushirikiano mkubwa wa kuboresha huduma Kwa wagonjwa wote wanaofika MOI

About the Author

You may also like these