Watumishi 25 wapongezwa kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja MOI.

Na Stanley Mwalongo- MOI

Ijumaa Octoba 06, 2023

Watumishi 25 wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wametunukiwa vyeti vya utoaji wa huduma bora kwa wateja katika mahadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja

Vyeti hivyo vilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Prof Abel Makubi ambapo alizipongeza kurugenzi mbalimbali, wakuu wa vitengo, mameneja pamoja watumishi na kuhimiza kuendelea kufanaya kazi kwa bidii ili kuifikisha MOI mbali zaidi.

“Watumishi wa MOI wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii sana, naomba nitumie nafasi hii leo kuwapongeza watumishi wote wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI) kwa huduma zao nzuri, huduma hizi bora ndio zinatufanya sisi pamoja na wagonjwa wote waliopo MOI kunufaika”

Sanjari na utoaji wa vyeti MOI ilisherehekea maadhimisho hayo kwa kula keki pamoja na baadhi ya wagonjwa kuashiria ushirikiano mzuri baina ya taasisi, watumishi na wateja wake.

About the Author

You may also like these