Patient Testimonial

Watu walisema sitainuka tena, Nilipoinuka wakasema sikuumia sana, walisahau kuna MOI

“Watu walisema sitainuka tena, kila mmoja aliamini maisha yangu yatakuwa ya kitandani tu, baada ya kupata ajali ya gari na kupata jeraha katika uti wa mgongo…nilipoinuka wakasema sikuumia sana” anasimulia Talick Elian Mbiza mkazi wa Jijini Dar es Salaam aliyetibiwa na kupona jeraha la uti wa mgongo katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Anasema “Nilipata ajali mwezi wa Sita mwaka huu ya kuburunzwa na gari nikiwa nyumbani kwangu na kusababishia maumivu ya uti wa mgongo…nililetwa MOI na kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo na sasa nimepona… namshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboreha huduma za afya nchini”

About the Author

You may also like these