watoto 24

Watoto 24 wamefanyiwa upasuaji katika kambi maalum

Na Mwandishi wetu- MOI

Zaidi ya Watoto 20 wenye Vichwa vikubwa na mgongo wazi wamefanyiwa upasuaji katika kambi maalum iliyoendeshwa na Madaktari bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ( MOI)

Hayo yamebainishwa leo na Daktari bingwa wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu kutoka MOI Dkt. Hamisi Shaban wakati akihitimisha kambi hiyo.

Dkt. Shaban amesema katika kambi hiyo wamefanikiwa kumfanyia upasuaji mtoto mwenye umri mdogo zaidi wa wiki moja.

“Siku ya Leo tumewafanyia upasuaji watoto 24 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi na wote wametibiwa na hali zao zipo vizuri” amesema Dkt. Shaban

Kwa upande wake mtaalam wa dawa za ganzi na usingizi Bw. Juma Said amesema wamehakikisha wagonjwa wamepata huduma ya dawa za usingizi na kufanyiwa upasuaji salama na wote wamepelekwa wodini.

Kambi hiyo imefadhiliwa na Mama Mariam, Zeenat kwa kushirikiana na Taasisi ya MOI.

About the Author

You may also like these