Wataalam MOI wajengewa uwezo kuimarisha huduma kwa wagonjwa wa dharura.

Na Mwandishi Wetu, MOI- Ijumaa Oktoba 10, 2023

Jumla ya Wataalam 55 wa Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) wamepatiwa mafunzo kwa vitendo ya kuimarisha huduma kwa wagonjwa wa dharura na mahututi, ili waweze kutoa huduma bora kwa haraka na ufanisi.

Akifunga mafunzo hayo Oktoba 9, 2023 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mkurugenzi wa huduma za Tiba Shirikishi Dkt. Asha Abdul amewahimiza wataalam hao kuhakikisha wanatoa huduma bora na kwa haraka kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ya dharura.

“Wauguzi, wataalam wa maabara, Radiolojia, Wafiziotherapia wamepatiwa haya mafunzo ili waweze kugundua haraka mgonjwa anapopata dharura, na pia kujifunza kwamba kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuweza kutoa huduma kwa wakati” amesema Dkt. Asha na kuongeza kuwa

“Pia wamejifunza ujuzi tofauti wa kuhumudumia mgo njwa atakayepata matatizo ya kupumua au wale wagonjwa wenye matatizo ya ubongo na mgongo, mafunzo haya yatawawezesha watoa huduma kutoa hudma wakiwa na ujasiri na kutoa matokeo chanya”

Washriki wa mafunzo hayo wamesema “Mafunzo haya yanaenda kuongeza ufanisi kwa sisi waunguzi katika kuwasaidia, lakini pia yametujengea uwezo sisi kama mabalozi kwenda kuwapa ujuzi wenzetu waliopo wodini ili kwa pamoja tuboreshe huduma” amesema Geofrey Kelimba

Kwa pande wake mkufunzi wa mafunzo hayo ya siku mbili, Hamisi Shafii amebainisha kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kutoa msaada wa huduma za dharura zinapohitajika katika maeneo yao ya kazi.

About the Author

You may also like these