Asilimia 75 ya wagonjwa wa Kibiongo huchelewa kuanza matibabu MOI.

Na Mwandishi Wetu-MOI

Zaidi ya asilimia 75 ya wagonjwa wa Kibyongo wanaofika Taasisi ya Tiba ya Mifupana Ubongo Muhimbili (MOI) kwa ajili ya matatibu hufika wakiwa wamechelewa hivyo kuathiri mwenendo wa tiba dhidi ya tatizo hilo.

Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Lemeri Mchome amesema hayo leo Novemba 6, 2023 wakati wa ufunguzi wa washa ya teknolojia bora ya kutibu Kibyongo iliyowashirikisha madaktari wa taasisi hiyo iki wezeshwa na wataalam kutoka Palestina na Paksitani

Dkt. Lemeri amesema ni wakati sasa kwa jamii kujenga utamaduni wa kuwapeleka watoto wenye Kibyongo hospitali mapema ili waweze kupatiwa tiba sahihi na kuendelea kukua na kuishi bila changamoto hiyo.

“Wenzetu wamekuwa na teknolojia ya kuanza kuunyosha mgongo kwa kuwekea vyuma kwa nje na baadaye kufanya upasuaji…teknolojia hii itamfanya mtu aliyeishi na kibyongo kwa mda mrefu aweze kusimama vizuri” amesema Dkt. Lemeri

Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Palestine Prof. Alaa Ahmad amesema mafunzo hayo ya siku tatu yanalenga kuwajengea uwezo wa kitaalam madktari wa MOI kuweza kutibu tatizo la Kibyongo kwa njia za kisasa, ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano uliodumu kwa miaka minne sasa.

Mratibu wa mafunzo hayo Dkt. Bryson Mcharo amebainisha kuwa jitihada hizo zinalenga kuifanya MOI kuwa kituo bora cha tiba za mifupa Afrika Mahsariki, Magharibi na ya Kati.

“Hapa wataalam wetu wnajengewa uwezo na namna ya kutibu Kibyongo cha muda mrefu, kibyongo ambacho hakijatibiwa kwa muda mrefu kiasi ambacho mgonjwa wakati mwingine anashindwa hata kupumua” amesema Dkt. Mcharo
mwisho

About the Author

You may also like these