Kaimu Mkurugenzi mtendaji MOI

Wahitimu dawa za usingizi MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ilitoa vyeti kwa wanafunzi 50 waliohitimu mafunzo ya miezi sita kutoa dawa za usingizi na ganzi Katika ukumbi wa mikutano MOI.

Dkt. Swai aliwapongeza wanafunzi hao kwa kuhitimu mafunzo hayo na kuwataka wakatumie mafunzo waliyoyapata MOI kutoa huduma katika hospitali mbalimbali zilizopo nchini ili kupunguza uhaba wa Wataalam hao.

“Kozi hii imefanikiwa sana kwani wanafunzi 50 wametunukiwa vyeti kati ya Wanafunzi 51, na hii ni heshima na mafanikio makubwa sana kwa taasisi yetu ya MOI, siku za usoni tunategemea kuiboresha kozi hii ili tuzidi kuongeza idadi ya Wataalam hawa kwani hapa nchini ni wachache sana.”

Mhitimu wa kozi hiyo Bw. Gido Damas aliushukuru uongozi, jumuiya na wakufunzi wa MOI kwa kutoa mafunzo ambayo yamewapa maarifa mapya.

About the Author

You may also like these