wagonjwa na ndugu wa wagonjwa wanaopata matibabu MOI waaswa kuwa huru kutoa maoni

Na Amani Nsello-MOI

Wagonjwa na ndugu wa wagonjwa wanaopata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wameaswa kuwa huru kutoa maoni yao ili yatumike kama nyenzo ya kuboresha hduma zaidi.

Wito huo umetolewa jana Jumatano Oktoba 02, 2024 na Meneja Uhusiano kwa Umma wa MOI Patrick Mvungi wakati akiongea na wagonjwa na ndugu wa wagonjwa maeneo mbalimbali ya taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya madhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

“Msiwe na hofu kutoa maoni, kwani huduma hizi tunazozitoa ni kwa ajili yenu, hivyo maoni yenu ni dira kwetu ya kufanyia tathimini kwenye kuboresha huduma zetu”. Amesema Mvungi

Mvungi amesema kuwa katika wiki hii ya huduma kwa wateja watatembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma katika taasisi hiyo ili kuweza kupokea maoni kutoka kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa kwa ajili ya kuboresha huduma za matibabu.

Kwa upande wake muuguzi kutoka kitengo cha Udhibiti Ubora wa MOI Zaituni Bembe amesema kuwa katika wiki ya Huduma kwa Wateja licha ya kuwasikiliza wagonjwa na ndugu wa wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika taasisi hiyo, lakini pia watawasikiliza watumishi wa taasisi hiyo ambao wanapatiwa matibabu na wataalam wa afya wa taasisi hiyo ili kuweza kupata mrejesho wa huduma zao za matibabu.

About the Author

You may also like these