Na Mwandishi wetu- Dodoma
Waheshimiwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameipongeza Taasisi ya tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kusogeza huduma za kibingwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na maboresho makubwa yanayofanyika katika Taasisi ya MOI.
Pongezi hizo zimetolewa na Wabunge hao waliotembelea banda la MOI liliopo katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wabunge hao wameipongeza Menejimenti ya Taasisi ya MOI kwa kusogeza huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu katika viwanja vya Bunge hilo kuanzia tarehe Januari 29 hadi 2 februari 2024
Pia ,wamepongeza uanzishwaji wa huduma ya wagonjwa mashuhuri na wa kimataifa (Premier and International Patients Services)
Aidha Wabunge hao wameuomba uongozi wa MOI uendelee kusogeza huduma za kibingwa Bungeni Mara kwa Mara ili kuwapa taarifa waheshimiwa Wabunge kuhusu fursa ya huduma za kibingwa zinazopatikana hapa nchini.