Simu za upepo (Radio call) kuanza kutumika ndani ya hospitali ya MOI ili kurahisisha mawasiliano katika ubora wa huduma.

Na Mwandishi wetu- MOI, 7 Agosti, 2023 Dar es salaam

Simu za upepo (Radio Call) zitaanza kutumika rasmi katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo MOI kwa lengo la kurahisisha mawasiliano miongoni mwa watumishi na viongozi wao ili kuboresha huduma kwa wagonjwa na kuongeza kasi ya uwajibikaji.

Hayo yamebainishwa katika kikao baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Profesa Abel Makubi na wakurugenzi wote, watumishi wa vitengo vya udhibiti ubora , mapokezi, huduma kwa wateja, Usalama na wakuu wa idara za Radiolojia, wagonjwa wa nje na ndani, maabara na kitengo cha dharura.

“Tumenunua simu ambazo kila Mkurugenzi, wakuu wa Idara, watoa huduma kwa wateja pamoja na walinzi watakuwa nazo, lengo ikiwa ni kurahisisha uratibu na mawasiliano pia kujua kila kinachoendelea MOI kwa gharama ndogo na kwa urahisi” Wahudumu watakuwa na uwezo wa kupeana taarifa fupi za wagonjwa na kuwahi kufika kutoa hudumu huku viongozi pia wakifatilia kupitia simu hizo za upepo; Alisema Prof. Makubi

Kwa upande mwingine Prof. Makubi amewapongeza watumishi wa kitengo cha Usalama pamoja usafi kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya.

“Niwaombe watumishi wa idara nyingine muige mfano wa idara za ulinzi na usafi, nawaomba kila mtu abadilike na tuboreshe huduma kwa wateja wetu, mgonjwa akija MOI apate huduma na aridhike, tujifunze kuwa na lugha za Pole na karibu kwa wateja wetu” Alisema Prof.Makubi

Prof. Makubi amewataka watoa huduma wote kutozuia kuwapa namba za simu wananchi wapatao huduma MOI kwa lengo la kujua maendeleo ya mgonjwa akiwa ndani hata nje ya MOI

About the Author

You may also like these