Vifaa vipya

Serikali yaongeza mashine za MRI na CT SCAN MOI

NA Mwandishi Wetu MOI, Jumapili Oktoba 15, 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Prof. Abel Makubi amesema Serikali ya awamu ya sita inaboresha Huduma za uchunguzi kwa kuongeza mitambo mipya mingine ya vipimo vya MRI na CT Scan (hivyo kuwa MRI 2, na CT 2) ambayo itaondoa kero ya wananchi kutumia muda mrefu kusubiri huduma hiyo.

Akizungumza leo Jumapili Oktoba 15, 2023 wakati wa ziara ya menejimenti ya MOI ya katika kitengo cha dharura, wodini, mradi wa mashine ya kipimo cha MRI na CT Scan na eneo la kusubiria wagonjwa kitengo cha dharura amesema kuanza kazi kwa mashine hizo kutaondolea adha ya wagonjwa kusubiri kwa muda mrefu.

Prof. Makubi amesema kuwa mashine za MRI na CT Scan zinatakiwa zianze kazi mapema November 2023 ili kuondoa adha ya wagonjwa kusubiri kwa muda mrefu”

About the Author

You may also like these