Na Erick Dilli- DODOMA
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imetembelea shule ya sekondari Mnadani jijini Dodoma na kuwapa elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza kwa wanafunzi na walimu shuleni hapo.
Elimu hiyo imetolewa leo tarehe 12 Novemba, 2024 na mtaalam wa Magonjwa ya ndani kutoka Taasisi ya MOI, Dkt. Doreen Watugulu ambaye ameushukuru uongozi wa shule hiyo kwa kutoa fursa kwa anafunzi kupata elimu hiyo.
“Nashukuru kwa namna wanafunzi pamoja na walimu walivyojitokeza ili kupata elimu kuhusu magonjwa haya yasiyambukizika kwani ni vyema kujua chanzo, dalili pamoja na njia za kujikinga…moja ya njia kubwa ya kukabiliana nayo ni kufanya mazoezi na kuzingatia mlo sahihi, magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu hayaambukizi” amesema Dkt. Watugulu na kuongezea
Naye mwanafunzi wa shule hiyo, Amina Salehe amewashukuru wataalamu kutoka MOI kwa kuwatembelea na kuwapa elimu hiyo ya magonjwa yasiyoambukiza na kuahidi kutumia elimu waliyoipata kuifanyia kazi.
Elimu hiyo iliambata na vipimo vya presha pamoja na kisukari katika shule hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza