MOI yasogeza huduma za kibingwa bungeni

Na Mwandishi wetu- Dodoma.

Taasisi ya tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imesogeza huduma za kibingwa za Mifupa, Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dodoma.

Huduma hizo zimeanza kutolewa tangu tarehe 29 Januari na kufikia tamati 02 februari 2024.

Utoaji wa huduma hizo unaenda sambamba na utangazaji wa huduma mpya ya wateja mashuhuri na wakimataifa inayopatikana katika Taasisi ya MOI pamoja na utalii tiba.

About the Author

You may also like these