menejimenti MOI yakagua maeneo mbalimbali ya utoaji huduma na kutatua changamoto

Na Abdallah Nassoro-MOI

Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) ilifanya ukaguzi mkubwa (grand round) katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ili kupima uwajibikaji wa watoa huduma katika maeneo yao ikiwamo suala la usafi, kufuata miongozo (SOPs) na hali ya miundombinu.

Ukaguzi huo uliofanyika Oktoba, 29, 2024 uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Laurent Lemeri Mchome ambaye aliwapongeza watoa huduma kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa na kuwahimiza kuzingatia miongozo ya utoaji huduma kwa kila kada.

“Hakikisheni miongozo ya utoaji huduma (SOPs) kwa kila ofisi inabandikwa ukutani, siku hata kama wewe haupo akija mtumishi mgeni bado ataweza kufanya kazi sawa na wewe kwa kuzingatia miongozo ya kazi iliyowekwa” alisema Dkt. Lemeri

Aliongeza kuwa “Tuendelee kufanya kazi kwa bidi na maarifa makubwa ili tuwasaidie wagonjwa wetu wapone haraka na warejee katika shughuli zao za ujenzi wa Taifa…tunawapongeza watoa huduma kwa kufanya kazi kwa bidii na tunawaomba zile kasoro ndogondogo zirekebishwe, na yale ya upande wetu niwaahidi tutayafanyia kazi kwa haraka”

About the Author

You may also like these