Na Mwandishi wetu- MBEYA
Wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake wameendelea kupata huduma katika banda la Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili MOI katika Maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa 2025 inayofanyika jijini Mbeya.
Kilele Cha maadhimisho hayo yaliyoambatana na maonesho yanafanyika katika kiwanja cha uhindini jijini Mbeya leo Oktoba 10, 2025.
Afisa Muuguzi Mwandamizi MOI Bw. Fidelis Gakuba amesema wananchi wananufaika na ujio wa MOI katika maadhimisho hayo.
“Katika Banda letu (MOI) wananchi wanapata fursa ya kuhudukiwa na Madaktari bingwa na bobezi wa Mifupa, Ubongo, Mgongo pamoja na Mishipa ya Fahamu lakini pia kuna huduma ya Mazoezi Tiba” amesema Bw. Fidelis na kuongezea
“Huduma hizi zote zinatolewa bure hivyo wananchi waendelee kujitokeza katika banda letu”
Aidha, Mkazi wa jiji la Mbeya Bw. chris Misasambili amefurahishwa na uwepo wa Taasisi ya MOI kusogeza huduma zake karibu na wananchi.
Maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa 2025 imeanza Tarehe Oktoba 08, 2025 na kutamati Oktoba 14, 2025 ikibebwa na kauli mbiu Nguvu kazi ya vijana kwa Maendeleo Endelevu, Taasisi ya MOI itakuwepo siku zote kuhudumia wananchi. Karibuni sana.