Baraza la wafanyakazi MOI lampongeza Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala

Na Abdallah Nassoro – MOROGORO

Kikao cha kwanza cha Baraza la Sita la Wafanyakazi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), limeazimia kumpongeza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala (DAHRM), Orest Mushi kwa jitihada zake katika kuhakikisha watumishi wa taasisi hiyo wanapata haki na stahiki zao kwa wakati.

Azimio hilo limefikiwa leo Ijumaa Machi, 14, 2025 katika kikao kinachoendelea Hoteli ya Edema mjini Morogoro ambapo baraza hilo kwa kauli moja limeazimia kumpongeza mkurugenzi huyo wa rasilimali watu na utawala.

“Nashauri baraza hili litoe azimio la kumpongeza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala (DAHRM) kwa kazi kubwa anayoifanya ya kushughulikia kwa wakati haki na stahiki za watumishi” amesema Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI

Wazo hilo liliungwa mkono na wajumbe wa baraza hilo la wafanyakazi kwa kauli moja na hivyo kuwa azimio halali la kumpongeza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala (DAHRM) Orest Mushi.

About the Author

You may also like these