Na Erick Dilli- Dodoma
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inashiriki katika maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibi magonjwa yasiyoambukiza yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Squre jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yamefunguliwa leo Novemba 9, 2024 na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu ambaye amewataka watanzania kubadili mitindo ya maisha kwa kujiepusha tabia bwete ili kuzuia magonjwa hayo.
“Wizara ya Afya itaendelea kuwahakikishia Watanzania afya njema kwa kutoa elimu na ushauri juu ya magonjwa yasiyoambukiza ili kuleta maendeleo binafsi na Taifa kwa ujumla…ni muhimu kujiepousha na tabia bwete kwa kufanya mazoezi na kuzingatia ulaji bora” amesema Dkt. Jingu
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Alhaji Jabir Shekimweri amewapongeza Wananchi wote waliojitokeza katika mazoezi na kugusia juu ya umuhimu wa mazoezi dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.
Tatika maadhimisho hayo Taasisi ya MOI inatoa huduma za ushauri wa lishe bora, magonjwa ya mifupa, ubongo namishipa ya fahamu na vipimo bure vya magonjwa ya moyo.
Maadhimisho ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza yameanza leo Novemba 9, 2024 na yatatamatika Novemba 16, Jijini Dodoma ambapo ushauri na elimu utatolewa bure