Na Lindarachel Kasuke –MOI Ijumaa Oktoba 6,2023
Katika kuadhimisha kilele cha wiki ya huduma kwa wateja, Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imesherehekea na wagonjwa ambapo walikata keki na kula pamoja ikiwa ni ishara ya upendo na mahusiano mema baina yao.
Kwenye hafla hiyo Mkurungezi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi alikata na kuwalisha keki wagonjwa kuonyesha ishara ya upendo, kuwathamini na kuwajali.
“Ni wajibu wetu kumuhudumia kila mgonjwa awe tajiri, awe masikini tumejitahidi kupunguza muda wa kusubiri kupata huduma, kazi yetu Mungu ametupa sisi ni kuchelewesha kifo ; sisi watalaamu tukiongeza hata siku moja ya uhai kwa mgonjwa, tunashukuru Mungu;amesema Prof. Makubi
Mmoja wa wagonjwa walioshiriki kula keki na watumishi wa MOI, Zuwena Abdallah ameipongeza taasisi kwa kuboresha huduma na kwamba kitendo cha kuwalisha keki wagonjwa na kufurahi pamoja kimezidi kuwafariji.