Waziri wa afya zanzibar Mhe. Mazuri aipongeza MOI kwa huduma nzuri

Na Stanley Mwalongo- ZANZIBAR

Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui ameipongeza Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kutoa huduma bora za matibabu ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kwa wanachi wa Zanzibar wanaotibiwa MOI.

Mhe. Mazrui ameyasema hayo siku ya Jumanne Mei 06, 2025 alipotembelea banda la MOI katika maonesho ya Wiki ya Afya Zanzibar, yanayofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar.

“ Naipongeza Taasisi ya MOI kwa kutoa matibabu bora kwa wananchi wa Zanzibar wanaokuja kutibiwa magonjwa ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu katika Taasisi yenu” amesema Mhe. Mazrui

Aidha, Mhe. Mazrui ameishukuru MOI kwa kushiriki katika maonesho hayo yaliyoanza tarehe 4 Mei ambayo yatafikia tamati 10 Mei 2025 Zanzibar.

About the Author

You may also like these