Na Erick Dilli- MOI
Wauguzi wapya katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wapatiwa mafunzo ya kanuni na miongozo wa utendaji kazi katika Chumba cha upasuaji.
Mafunzo hayo yanafanyika leo septemba 13, 2025 kupitia Taasisi ya AO Alliance ya nchini Uswisi kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) ambapo Mratibu wa Mafunzo hayo Bi. Mariam kumbwani ameeleza lengo la Mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wauuguzi wapya katika Taasisi hiyo
“Lengo la Mafunzo haya ni kuwafundisha kanuni na miongozo ya utendaji kazi wakati wakiwa katika Chumba cha Upasuaji ili kuhakikisha ubora wa utoaji huduma kwa wagonjwa wetu” na kuongezea
“Tumeanza kuwapa mafunzo ya vifaa vinavyotumika kwa wagonjwa wanaopata mivunjiko mikubwa ya mifupa kwenye mkono, paja na Mguu na siku za mbeleni tutaendelea kuwapa kanuni na Miongozo ya huduma zingine katika Chumba cha Upasuaji”
Afisa Muuguzi Msaidizi MOI Jesca Mkwaka ameshukuru Waratibu ya Mafunzo haya na kuahidi utendaji kazi ulio bora zaidi
“Kwa niaba ya wauguzi wenzangu tunashukuru kwa kupatiwa mafunzo haya ya kanuni na miongozi ya utendaji kazi katika chumba cha upasuaji tunaahidi kusimamia tuliyojifunza hapa ili kuhakikisha Taasisi inazidi kutoa huduma bora kwa wananchi”