Na Amani Nsello- KAWE
Watumishi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’ 2025 yenye Kauli mbiu ‘Uchaguzi Mkuu 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki’.
Maadhimisho hayo yamefanyika Kimkoa katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam, ambapo Katibu wa TUGHE MOI, Dkt. Paul Ruge ameushukuru Uongozi wa MOI kwa kuendelea kuwapa ushirikiano wao kama viongozi katika kutimiza majukumu yao.
“Tunaushukuru uongozi wa MOI kwa kuendelea kushirikiana nasi viongozi wa Wafanyakazi wa TUGHE katika tawi letu la MOI, tunaomba waendelee na ushirikiano huo katika kutimiza majukumu yetu ya kila siku”. amesema Dkt. Ruge
Aidha, Dkt. Ruge ameomba Serikali kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi sambamba na kuboresha miundombinu ya mahali pa kazi ili kuleta tija kazini.
Pia, Dkt. Ruge ameshauri Mamlaka zinazohusika katika kuratibu, kuandaa na kusimamia Uchaguzi Mkuu 2025, wahakikishe kuwa Uchaguzi unakuwa huru na wa haki ili kupata viongozi watakaotetea maslahi na changamoto za wafanyakazi.
Kwa upande wake, Bi. Fariji Ngulube, Mwandishi Mwendesha Ofisi Mwandamizi wa MOI, amesema kwamba wataendelea kuutumikia umma wa Watanzania kwa uaminifu, bidii na weledi