Na Erick Dilli – Geita
Wananchi 526 wanufaika huduma za ushauri wa matibabu kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) katika Maonesho ya nane ya kitaifa ya teknolojia ya madini jijini Geita
Maonesho hayo yametamatika leo Septemba 28, 2025 katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mjini Geita ambapo Daktari kutoka kurugenzi ya ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu MOI Dkt. Kenneth Mgidange ameeleza kuwa wananchi wengi waliopata huduma katika Banda la MOI wanasumbuliwa zaidi na tatizo la mgongo, mishipa ya fahamu, Nyonga na magoti.
“Wananchi wengi tuliowaona wanachangamoto ya Mgongo , Nyonga, Magoti na mishipa ya fahamu hivyo tuliwapatia matibabu kwa kushauri dawa za kutumia, wengine tuliwapa rufaa kwenda chato kwenye kliniki yetu na wengine kuja MOI ili waweze kuondokana na maumivu hayo” amesema Dkt. kenneth
Kwa upande wake, Mmoja wa Mkazi wa Geita Bi. Sarafina Joseph ameishukuru Taasisi ya MOI kwa kuanza kushiriki maonesha haya katika mkoa huu
“Tunashukuru MOI kwa kuleta huduma hizi karibu na wananchi wa ukanda wetu katika Maonesho haya, kiukweli tumefarijika kwa Matibabu na Mwakani tunawasubiri” amesema Bi. sarafina
Maonesho haya yalianza Septemba 18, 2025 na kutamati Septemba 28, 2025 ikibeba kauli mbiu “Ukuaji wa Sekta ya Madini ni matokeo ya matumizi ya teknolojia sahihi na uongozi bora, Shiriki uchaguz Mkuu Oktoba 2025”