Wakazi wa mbagala wakoshwa na huduma za kibingwa za MOI

Na Amani Nsello- MBAGALA

Wakazi wa Mbagala wamefurahishwa na huduma za kibingwa na kibobezi zilizotolewa na wataalam wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) katika kambi maalum ya matibabu iliyoandaliwa na Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Wa Adiventista Wasabato Tanzania (ATAPE).

Wakazi Mbagala wamebainisha hayo katika ukumbi wa Dar Live, Jijini Dar es Salaam Mei 14, 2025 ambapo wameeleza jinsi walivyoridhishwa na huduma nzuri na bora za matibabu waliyopewa na MOI.

Bi. Salma Ramadhan mkazi wa Mbagala amesema huduma za kibingwa na kibobezi za wataalam hao na akiomba kambi za namna hizi ziwe endelevu.

“Nimefurahishwa na huduma za madaktari wa MOI, huwa nasumbuliwa na maumivu ya mgongo kwa muda sasa, nilivosikia kuwa madaktari watakuwepo hapa Dar Live nikasema lazima nije kutibiwa, zoezi liwe endelevu hata mara moja kwa mwezi sio mbaya” alisema Bi. Salma

Naye, Mkazi wa Mbagala Bw. Omary Abdallah aliwapongeza waandaaji wa kambi hiyo ambao ni ATAPE na kuwashukuru kwa kufanikisha kambi hiyo ya matibabu ya afya bure.

Kwa upande wake, Mratibu wa kliniki jongefu MOI, Dkt. Bryson Mcharo amesema wakazi wa Mbagala wamekua na mwamko mkubwa wa kupata matibabu kwani kwa siku walikuwa wanaona zaidi ya watu 70.

About the Author

You may also like these