Na Abdallah Nassoro-MOI
Timu ya tathimini na udhibiti wa viashiria vya hatari ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeanza mafunzo ya siku tano ya kuanisha, kuchambua na kupendekeza njia za kukabiliana na viashiria vya hatari ili kuiwezesha taasisi kufikia malengo yake.
Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Julai, 16, 2025 na Meneja Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa MOI Bw. James Sibale kwa niaba ya Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, ambaye amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kubainisha viashiria vya hatari vya taasisi.
“Ni jukumu letu wajumbe kuhakikisha mafunzo haya yanakuja na nyaraka muhimu ya taasisi, rejesta itakayoainisha viashiria vya hatari vya taasisi, kupima uzito wake na namna ya kukabiliana ili kuiwezesha taasisi kufikia malengo yake” Bw. Sibale amsema na kuongeza kuwa
“Ni nyaraka muhimu kwa ustawi wa taasisi yetu hivyo ni lazima tuwe makini katika kitengeneza ili mchakato wa kuipitisha uwe rahisi, nyaraka tutakayoitengeneza itapelekwa kwenye menejimenti na baadaye bodi ya wadhamini kabla ya kuwa nyaraka halali ya MOI”
Mratibu wa mafunzo hayo Getudusy Myayau amesema wajumbe kutoka kila kitengo na idara za taasisi ya MOI wanashiriki mafunzo hayo muhimu ya kuandaa rejista ya viashiria vya hatari vya taasisi na namna ya kukabiliana navyo.
“Mwisho wa mafunzo haya tunatarajia kuwa na rejista ya viashiria vya hatari vya taasisi na ndiyo maana tumechukua mjumbe kutoka kwenye kila kitengo na idara ili watusaidie kuainisha viashiria vya hatari katika maneono yao ya kazi na hatmaye tupate viashiria vya hatari vya taasisi” amesema Myayau