Wagonjwa 540 wanapatiwa matibabu ya kibingwa mbeya

Na Abdallah Nassoro- MBEYA

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imefanikiwa kutoa matibabu ya kibingwa kwa wagonjwa 540 katika mkutano wa 109 wa washitiri wa elimu kwa umma unaomalizika leo Jijini Mbeya.

Daktari Bingwa wa Mifupa MOI Dkt. Tumaini Minja amesema wagonjwa wengi waliofika kwenye banda la MOI kupata huduma wamebainika kuwa na wanachangamoto za mifupa, nyonga, magoti, mgongo , magonjwa ya ndani na Ubongo.

“Zaidi ya 100 wamepewa rufaa ya kwenda MOI na wengine wamepewa rufaa kwenda hospital ya rufaa ya kanda Mbeya” amesema Dkt. Minja na kufafanua kuwa

“Wale waliopewa rufaa ya kwenda MOI tumebaini wanahitaji vifaa tiba, miundombinu na teknolojia ya juu pamoja na utaalam wa kibobezi ambapo vyote vinapatikana MOI”

MOI imekua ikitekeleza kwa vitendo agizo la Serikali ya awamu ya sita kwa kusogeza huduma zake za kibingwa na kibobezi karibu na wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kuwapunguzia adha ya kufuata huduma hizo MOI.

Taasisi ya MOI imefanikisha kambi hiyo kwa ushirikino na hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya (MZRH).

About the Author

You may also like these