Wafamasia MOI waadhimisha siku yao kwa kutoa msaada kwa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi

Na mwandishi wetu – MOI

Watumishi wa kada ya Famasia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wameungana na wenzao kote nchini kuadhimisha siku ya Mfamasia Duniani kwa kutoa msada wa kibinadamu kwa watoto wenye ulemavu wa kichwa kikubwa na mgongo wazi waliolazwa kwa matibabu hospitalini hapo.

Mkuu wa kitengo cha famasi MOI Bw. Francis Nsee amesema msaada huo wa chakula na mahitaji mengine muhimu kwa watoto hao umelenga kuendelea kuwafariji na kuwatia moyo wazazi wanaouguza watoto hao kama sehemu ya kuidhimisha siku hiyo.

“Leo ni siku ya Mfamasia Duniani, tunaadhimisha siku hii huku tukitoa wito kwa wagonjwa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa ili kuepuka madhara yanayotokana na mtumizi yasiyo sahihi ya dawa hizo…pia sisi wafamasia tumetoa msaada kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi” amesema Nsee na kuongeza kuwa

“Ni muhimu pia kwa wananchi wakafahamu kuwa yeyote anayepata changamoto inayohusiana na dawa au vifaa tiba, aje famasi kwa ajili ya kupata ufafanuzi na sisi yupo tayari kuwahudumia”

Septemba, 25, 2025 ni siku ya Mfamasia Duania na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Fikiria Afya, Fikiria Mfamasia”

About the Author

You may also like these