Tanznia yaongeza kasi huduma za usafirishaji na utalii tiba barani Afrika

Na Mwandishi Wetu- Zambia

Ubalozi wa Jamhuri a Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Zambia unaratibu ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya 97 ya Kilimo na Biashara ya Zambia ikiwa na lengo la kutangaza huduma za matibabu ya ubingwa bobezi zinazopatikana nchini pamoja na huduma za usafirishaji.

 Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Lt Gen Mathew Edward Mkingule amezikaribisha Taasisi kubwa tano za Tanzania zinazotoa huduma za usafirishaji na afya ambazo zimeshiriki katika maonesho hayo na hivyo Tanzania kupata nafasi ya kutangaza huduma inazozitoa kwa wananchi wa Zambia na washiriki wa maonesho hayo kutoka nchi mbalimbali mathalani za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.

Taasisi zinazoshiriki katika Maonesho hayo yanayoendelea hadi tarehe 4 Agosti, 2025 ni pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH)

About the Author

You may also like these