Na Abdallah Nassoro –Sabasaba
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Dkt. Marina Njelekela Julai, 7, 2025 ametembelea banda la MOI katika maonesho ya kimataifa ya 49 ya biashara, Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam na kuipongeza taasisi hiyo kwa kushusha gharama za matibabu ili kuwawezesha wananchi wengi kupata huduma za kibingwa na kibobezi za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.
Dkt. Njelekela amesema uamuzi wa kushusha ghalama za matibabu hadi Tsh. 5,000 kumuona daktari bingwa ni wa kupongezwa na kwamba umetoa fursa ya wananchi wenye kipato cha chini waliokuwa wanahitaji huduma za kibingwa na kibobezi lakini hawapati kutona na kushindwa kubudu gharama kuweza kupata huduma hizo katika banda la Sabasaba.
“Niwapongeze kwa uamuzi huu wa kushusha gharama za matibabu, sasa kwa Tsh. 5,000 tu mwananchi anapata huduma za kibingwa na kibobezi…usogezaji wa huduma hizi karibu na wananchi unalenga zaidi kuwapunguzia gharama za matibabu” amesema Dkt. Njelekela na kuongeza kuwa
“Muendelee kutangaza hizi huduma hapa Sabasaba nina amini wananchi wengi hawajapata taarifa hizi, ni jukumu letu kuhakikisha wananchi wanapata taarifa ili wazidi kujitokeza kwa wingi kupata matibabu haya, huduma munazotoa zinahitajika sana na wananchi wetu…nawapongeza watumishi wote waliokuja kutoa huduma katika banda hili, huduma ni nzuri na wanaonesha weledi kwa kile wanachowaeleza wananchi”
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi hiyo ya Wadhamini Bi, Zuhura Mawona amesisitiza umuhimu wa wananchi kupata taarifa juu ya ushiriki wa MOI katika maonesho hayo na huduma wamazotoa.
“Kuna elimu ya lishe bora inatolewa hapa, ni nzuri sana ili kujikinga na maradhi mbalimbali, elimu ya mifupa, mgongo, mishapa ya fahamu, mazoezi tiba na vipimo vya ultrasound vyote hivyo ninapatikana hapa banda la MOI” amesema Bi, Mawona
Meneja Uhusiano wa MOI, Bw. Patrick Mvungi amasema ujio huo wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini MOI umelenga kuona namna ambavyo taasisi hiyo inatoa huduma za kibingwa na kibobezi kwa wananchi na kuwatia moyo watumishi wanaotoa huduma katika banda hilo.