MOI yatunukiwa cheti cha kimataifa cha utoaji wa majibu bora ya sampuli za maabara

Na Amani Nsello- MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imetunukiwa cheti cha kimataifa cha utoaji wa majibu bora ya sampuli za maabara.

MOI imetunukiwa cheti hicho mapema Oktoba, 2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma kwenye Kongamano la 37 la kisayansi la wataalam wa maabara za Afya nchini Tanzania na kongamano la 23 la Kisayansi la Huqas pamoja na mkutano mkuu wa mwaka.

Msimamizi Mkuu wa maabara wa MOI, Nsiande Ndosi amesema kuwa kwa wao kutunukiwa cheti hicho ni deni kubwa kwao kwa kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora za majibu ya maabara kwa viwango vya juu na Kimataifa.

“Cheti hiki ni uthibitisho kuwa maabara yetu (Maabara ya MOI) inatoa majibu sahihi na ipo kwenye kiwango cha hali ya juu cha Kimataifa, kwa sababu tumefanya uchunguzi wa sampuli za kimataifa na kutoa majibu sahihi, tunaendelea kusonga mbele na kuhakikisha ubora huu unaendelea kuwa wa viwango vya juu”. Amesema Bi. Ndosi

Mgeni rasmi wa kongamano hilo alikuwa Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ambaye alisema kuwa kada ya wataalamu wa maabara imekuwa chachu ya utekelezaji maono ya Mhe: Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha watanzania wanapata huduma fungamanishi za afya

About the Author

You may also like these