MOI yatoa matibabu ya kibingwa na kibobezi ya mifupa mkoani arusha

Na Stanley Mwalongo- ARUSHA

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inashiriki katika kambi ya madaktari bingwa na wabobezi inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Kambi hiyo imeanza rasmi leo Juni 23, 2025 na itafikia tamati tarehe 29, Juni 2025, ambapo Madaktari bingwa wa MOI wanatoa huduma

za matibabu ya mifupa, nyonga, bega, maumivu ya mgongo na huduma ya fiziotherapia bure kwa wakazi wa Arusha na mikoa ya jirani.

Akizungumza wakati wa kambi hiyo Daktari bingwa wa mifupa MOI, Dkt. Emmanuel Lema amesema lengo la kushiriki kambi hiyo ni kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi za mifupa na fiziotherapia karibu na wananchi.

“Tumeshiriki kambi hii kwa kutoa matibabu bure ya kibingwa na kibobezi ya mifupa kwa wananchi wa Arusha na mikoa ya jirani ili kuwapunguzia adha na gharama ya kufuata matibabu hayo Dar es Salaam” amesema Dkt. Lema.

Ameongeza kwa kuwaaomba wananchi wenye matatizo mbalimbali ya mifupa kujitokeza kwa wingi katika kambi hiyo ili wapate matibabu bure.

Kambi hiyo imeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha huduma za kibingwa na kibobezi zinzasogezwa karibu na wananchi.

About the Author

You may also like these