MOI yasogeza huduma za kibingwa na kibobezi katika maonesho ya nane ya kitaifa ya teknolojia ya madini geita

Na Erick Dilli- Geita

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imesogeza huduma zake za kibingwa na kibobezi za Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu katika maonesho ya nane ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya nanenane mkoani Geita.

Akizungumza Septemba 19, 2025 Mkurugenzi Mtendaji MOI Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema lengo la kuanza ushiriki MOI ni kutoa fursa kwa wakazi wa mkoa wa geita na washiriki wa maonesho hayo kupata huduma za kibobezi za MOI

“Kama Taasisi tumeamua kushiriki kwenye maonesho haya kwani toka kuanzishwa kwake yamekua na muitikio mkubwa kwa wakazi wa Geita na mikoa jirani na hivyo Kama Taasisi tukaona ni vyema kusogeza Huduma zetu za kibingwa na kibobezi za Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu karibu na wananchi” amesema Dkt Mpoki na kuongezea

“Tunawakaribisha wananchi wote wa Geita na mikoa jirani kutembelea Banda letu ili kupata huduma za Madaktari bingwa wetu ambao watakua hapa kwa siku zote za maonesho”

Maonesho ya nane ya kitaifa ya kiteknolojia ya madini jijini Geita yameanza Septemba 18, 2025 na kutamati Septemba 28, 2025.

About the Author

You may also like these