MOI yasogeza huduma za kibingwa na kibobezi dodoma na mikoa jirani

Na Erick Dilli- DODOMA

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inashiriki wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika katika Kiwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.

Huduma zimeanza kutolewa leo Juni 16, 2025 katika kiwanja cha Chinangali Park, Dodoma ambapo Daktari Bingwa Mbobezi wa mifupa MOI, Dkt Tumaini Minja ameeleza huduma ambazo wananchi wanazipata katika banda la MOI.

“Katika wiki hii ya utumishi wa umma tunatoa huduma ya ushauri wa kibingwa na bobezi za Mifupa, Ubongo, Mgongo, Mishipa ya fahamu pamoja na utengamao” amesema Dkt Minja na kuongezea

” Jopo la Madaktari na Watalaam tupo hapa kwa ajili ya kuhudumia wananchi ikiwa ni sehemu ya utumishi bora”

Naye, Bw. Sharif Masoud, mkazi wa Bukoba amefurahishwa na huduma bora aliyoipata alipotembelea banda la MOI.

“Nilikuwa na shida ya mgongo kwa mda kidogo na nashukuru Madaktari na Wataalam kutoka MOI wapo hapa wamenipa huduma bora ambayo ntaifanyia kazi ili kuweza kuondokana na maumivu ya mgono” amesema Bw. Sharif

Wiki ya utumishi wa umma imeanza leo Juni 16, 2025 na itafikia tamati Juni 23, 2025 na Taasisi ya MOI itatoa huduma hizo bure wakati wa wiki hiyo. Karibu tukuhudumie.

About the Author

You may also like these