MOI yasogeza huduma za kibingwa bungeni

Na Stanley Mwalongo – Dodoma

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imesogeza huduma za kibingwa za ushauri wa magonjwa ya nyonga, maumivu ya mgongo, mifupa, ubongo, mishipa ya fahamu, fiziotherapia na famasia katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanzania, jijini Dodoma.

Akizungumza katika banda la MOI leo Juni 2, 2025 Daktari bingwa wa mifupa wa MOI Dkt. Shadrack Mwaibambe amesema watatoa huduma hizo za kibingwa kuanzia leo Juni 2, 2025 na kufikia tamati Juni 6, 2025.

“MOI tumesogeza huduma zetu za kibingwa za ushauri wa matibabu ya mifupa, ubongo, mgongo,mishipa ya fahamu na nyonga, huduma za fiziotherapia na dawa katika viwanja vya Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania”

Amesema utoaji wa huduma hizo unaenda sambamba na utangazaji wa huduma ya wagonjwa maalum na wakimataifa inayopatikana katika Taasisi ya MOI.

Kwa upande wake Mfiziotherapia mbobezi wa MOI Dkt. Marry Chandeu amesema wanatoa elimu ya kuepuka maumivu ya mgongo na nini cha kufanya pindi mtu anapogundua maumivu ya mgongo ya muda mrefu.
6:00 AM

About the Author

You may also like these