MOI yashiriki maonesho ya kitalii ya kimataifa

MOI YASHIRIKI MAONESHO YA UTALII YA KIMATAIFA.

Na Mwandishi wetu-MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeshiriki maonesho ya kimataifa ya utalii ikatika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ambaye aliipongeza MOI.

Mhe. Albert Chalamila amesema anatambua kazi kubwa inayofanyaa na taasisi ya MOI kwa kuhakikisha kila mwananchi anapatiwa huduma bora.

“Leo tunaongelea utalii na teknolojia kwa namna gani inaweza kuwa na unafuu katika maswala ya tiba hapa nchini zamani uvimbe wa chini ya ubongo ulikua unatibiwa na upasuaji lakini sasa tunatumia njia za pua amesema Chalamila.

Kwa upande mwingine Mratibu wa Tiba Utalii kutoka Wizara ya Afya, Asha Mahita amesema kwa mwaka huu wamepokea zaidi ya wagonjwa 5000 kutoka nchi mbalimbali kutokana na aina ya matibabu waliyonayo.

Naye Dkt.Anna Lemunge Mjumbe wa kamati ya tiba utalii MOI ameipongeza na kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya afya hapa nchini.

https://www.instagram.com/p/CyD6nratHAk/

About the Author

You may also like these