MOI yaokoa billioni 149.8 rufaa za matibabu nje ya nchi

Na Abdallah Nassoro- MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeokoa kiasi cha Tsh. 149.8 ambazo zingetumika na serikali kugharamia matibabu ya wagonjwa wa mifupa na ubongo , mgongo na mishipa ya fahamu wa rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi katika kipindi cha miaka minne ya uongozi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma leo Machi, 5, 2025 kuhusu mafanikio ya Taasisi ya MOI katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia suluhu Hassan.

Katika mkutano huo ulioandaliwa na Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Mpoki amesema Taasisi ya MOI imefanikiwa kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi za matibabu ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa a fahamu karibu na watanzania ambao awali walilazimika kufuata huduma hizo nje ya nchi.

Amesema uboreshaji wa miundombinu ya kutolea tiba, vifaa tiba na usomeshaji wa madaktari bingwa na wabobezi uliofanywa na serikali ya awamu ya sita umewezesha huduma nyingi za kibingwa za mifupa na ubongo kutolewa katika taasisi hiyo.

“Tumeanzisha huduma mpya za kibingwa na kibobezi 10 za matibabu ya mifuppa na ubongo, haya yote yamewezekana baada ya serikali ya Rais dkt. Samia Suluhu Hassan kuwekeza katika miundombinu, vifaa tiba vya kisasa na ujuzi kwa watalaam wetu” amesema Dkt. Mpoki na kufafanua kuwa

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa hakuna mgonjwa anayepewa rufaa nje ya nchi kutibiwa, kama mtu atahitaji kwenda nje basi aende kwa matakwa yake…huduma za kibingwa kama upasuaji wa ubongo, mgongo kwa njia ya matundu, ubadilishaji wa nyonga, magoti, matibabu ya kiharusi zinatlewa MOi kwa kiwango kilekile cha kimataifa”

Dkt. Mpoki amewataka Watanzania kuendelea kuiamini Taasisi ya MOI na kuwa kimbilio lao kwa matatizo ya mifupa, ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu na kiharusi na kwamba watalaam wapo tayari kutoa huduma bora kwa wagonjwa wote.

About the Author

You may also like these