Na Mwandishi Wetu- Pemba
Washiriki wa maonesho ya elimu ya juu yanayoendelea visiwani Pemba wamevutiwa na banda Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), ambapo wengi waliotembelea banda hilo kupata elimu juu ya huduma za kibingwa na kibobezi zinazotolewa wamepongeza.
Afisa uhusiano wa MOI Abdallah Nassoro amesema wengi wametembelea banda la MOI kwa lengo la kujifunza juu ya huduma matibabu ya kibingwa ya Mifupa, Ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu zinazotolewa na MOI.
Maonesho hayo yaliyoanza Julai, 14 ,2025 Unguja yatafikia tamati Julai 27, 2025 na kwamba MOI imeshiriki ili kutoa elimu kwa wananchi wa Pemba.
“Ni mara yetu ya kwanza kuja kutoa huduma na elimu katika visiwa vya Pemba, ikiwa ni mkakati wa Taasisi yetu wa kuwapa wananchi ya kuzifahamu huduma za kibingwa zitolewazo na MOI pamoja na kupata ushauri wa kitabibu” amesema Nassoro
Ameongeza kuwa “Wakazi wa Chakechake, Wete, Mkoani na viunga vyake waje kupata elimu ya Mifupa, Ubongo na viungo saidizi (bandia)